Tambua namna ADUI ANAVYOTUMI ARDHI AU ENEO UNALOISHI KUHARIBU MAISHA YAKO

*IJUE NAMNA AMBAVYO ADUI YAKO ANAVYOWEZA KUTUMIA ARDHI /NCHI UNAYOIKAA KUHARIBU MAISHA YAKO* 
ZEKARIA 18
18 Nami nikainua macho yangu, nikaona, na tazama, pembe nne.
19 Nami nikamwuliza yule malaika aliyesema nami, Nini hizi? Naye akanijibu, Hizi ndizo pembe zilizowatawanya watu wa Yuda, na Israeli, na Yerusalemu.
20 Kisha BWANA akanionyesha wafua chuma wanne.
21 Ndipo nikauliza Hawa wanakuja kufanya nini? Akasema kwamba, Hizi ndizo pembe zilizowatawanya watu wa Yuda, hata ikawa hakuna mtu aliyeinua kichwa chake; lakini hawa wamekuja kuzifukuza, kuziangusha pembe za mataifa, walioinua pembe yao juu ya nchi ya Yuda, ili kuwatawanya watu wake.
Bwana Yesu asifiwe sana sana 
Nilikuwa moshi kwenye mji wa familia moja ivi na nilipokaa pale nikawa nafanya maombi kwa ajili ya ile familia katika yale maombi pepo likalipuka pale na likajielezea kuwa limechukua nafsi ya mtu ambaye alikuwa analitaka eneo ambalo wanalolikaa ambalo Baba yao alipewa na Babu yao lakini huyu mtu mmoja akawa analitaka lote liwe lake ,na hili kulipata ilibidi kwanza auwe Baba wa familia na akachukua damu na akaweka agano kwenye ardhi yao kwamba kiwepo na kiti kwenye hiyo Ardhi au nchi ambacho atakuwa anakitumia kuwafunga na kuwaharibu kupitia hiyo Ardhi yao na akafanya jambo lingine pia akaweka roho ya mafarakano na chuki na malumbano kati ya wanandugu ,akahakikisha anawatawanya wote pale kwenye ile ardhi na hata ule usiku ,kilichokuwa kinawafanya walumbane na kujisikia uchungu na kilio kwa Dada mmoja ndani ya ile familia usiku ule ni kwamba yule Aliyekuwa anataka kuvuruga ile familia alikuja usiku alimtuma mke wake ili aje awavuruge ule usiku wasielewane 
Na likaeleza kuwa damu ya marehemu yaan baba mwenye nyumba na hirizi aliyokuwa nayo ndio inayompa uhalali wa kukamata ile ardhi na kuwavuruga na kuwagombanisha na kuwatawanya ni Sawa Sawa na ile Zekaria 1:18-19 inaeleza juu ya nabii Zekaria alivyopewa macho ya rohoni ya kuona shida au tatizo lilikuwepo kwenye nchi au ardhi ya Yuda na Yerusalemu anasema kuwa kulikuwepo na pembe ambazo ziliwatawanya watu wa Yuda na Yerusalemu na zikahakikisha awafanikiwi kwenye ardhi hizo kabisa ,ile Zekaria 1:21 inaeleza kuwa zile pembe zilizowatawanya Watu wa Yuda na Yerusalemu zilikuwa na nguvu za kuwagawa na kuwatawanya kiasi ambacho hawakuweza kuinua kichwa hata kidogo yaani ziliwafanya wawe dhaifu sana mbele ya hizo pembe 
Kiukweli ni kwamba kama hautaweza kuzishughulikia ipasavyo utashangaa ardhi unayoikaa inakuwa moto ,huwezi kuendelea na saa ingine unalazimika kuikimbia nyumba yako au nyumba yenu kabisa 
Na kama adui amekusudia kukumaliza anaweza kutumia ardhi kabisa ya kwenu kukufarakanisha na kukuwekea mikosi na umaskini ,kutokuolewa wala kuoa 
Ukisoma Zekaria 1:21 utaona kuwa inatakiwa Mungu atume malaika zake kuwafungua ,na kuzifukuza na kuangusha chini vile vimewekwa kwenye hiyo ardhi hapo ili maisha yapate kurejea kwa upya 
Katika maelezo ya lile pepo lilidai kuwa limepewa haki ya kukamata ardhi ya familia ya yule Dada lilisema pia lilitumia maneno kukamata ardhi na maisha ya watu wa ile familia na hili jambo ukisoma Yeremia 30:3-4 utaliona wazi wazi kuwa katika ulimwengu wa kiroho wakitaka kukamata Ardhi na maisha ya wakazi wa hapo wanatumia maneno ya kuwafunga na kuwatawanya wakaao juu ya hiyo ardhi ,wakiisha tumia maneno ya kuwatamkia ya kimaagano na kuhachia roho ya umaskini ,njaa ,magonjwa ,mafarakano ,vifo basi wanakuwa wamemaliza kazi sasa kama ujajua kwenda kwa Mungu na kuomba toba na rehema basi hali inakuwa mbaya sana kwenye familia 

Watahachia vitu vibaya kwenye ardhi kwa maneno ya kimaagano yenye roho yenye nguvu nyuma yake ya kutawanya ,kufarakanisha ,umaskini na n.k na hili kukomboa hiyo ardhi lazima utumie pia maneno na ndio maana Yeremia 30:4-9 inaeleza wazi kuwa Mungu alipotaka kuwakomboa Yuda alianza kutuma kwanza neno kwao na kwa adui zao la ukombozi ,neno linaweza kutumika kukomboa shida ya familia iliyofungwa na roho za kipepo kwenye ardhi 
Neno la Mungu na damu ya Yesu na jina pia ni ufunguo wa kufungulia ardhi na wanayoikaa pia

Leave a comment